Thursday, 1 March 2018

HII NDIO IDADI YA WANAUME ALIOTOKA NAO LINNAH

Msanii wa Bongo Fleva, Linah ameamua kuweka wazi kwa kutaja idadi ya wanaume ambao alishawahi kudate nao tangu awe maarufu huku akishindwa kukumbuka wanaume ambao alikuwa nao kipindi hicho kabla ya kupata jina.
Linah amesema tangu apate jina ametembea na wanaume watano tu mbali na mwanaume aliyezaa naye ambaye wananaishi pamoja kwa sasa.
“Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume watano hivi toka watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa,“amesema Linah kwenye mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni.
Hata hivyo, Linah amesema idadi hiyo ya wanaume ni baada ya kupata jina ila wale aliyowahi kutoka nao kimapenzi kipindi cha nyuma kabla ya umaarufu hawakumbuki ila ni kati ya 10 au 15.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search