Monday, 19 March 2018

IRENE UWOYA:-DOGO JANJA AMENIPA KITU AMBACHO WANAUME WENGI WAMESHINDWA KUNIPA

Msanii wa bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa wala hajali watu wanaosema kuwa amemzdi mwanaume aliyemuoa miaka mingapi kwa sababu yeye anachojali zaidi ni mapenzi na wala sio kitu kingine.


Irene Uwoya ameyasema hayo jana alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha Leo tena cha Clouds Radio alipokwenda yeye na mumewe huyo.


Irene anasema kuwa kwake umri ni namba tu kwa sababu hata kwa hao wanaume wenye kulingana nao umri hawakuweza kumpa kile alichokuwa anakitaka.


"Ni kweli nimemzidi umri na sio umri peke yake hata vitu vingine nimemzidi labda yeye kanizidi dhambi(Akiongea kiutani), Kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata.

"Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo“


Irene anakiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, dogo janja ndio mwanaume aliyeweza kumpa kitu ambacho hajawahi kupata kwa mwanaume yoyote na wala sio hela bali ni mapenzi ya dhati.


"Sijaolewa na dogo janja kwa sababu ya pesa,kuna vitu vingi ambavyo nimevutiwa kutoka kwake .Kwanza nilipenda mara ya kwanza alivyokuja na kuni-approch.Dogo Janja amenipa kitu ambacho wanaume wote niliokuwa nao walishindwa kunipa."

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search