Monday, 5 March 2018

Jaji Mutungi awakalia kooni CHADEMA. Awapa siku tano kuja na majibu yanayoridhisha!

[​IMG]
Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi

Barua hiyo ya Jaji Mutungi inatokana na kutoridhishwa kwake na majibu ya barua yake ya Februari 21, 2018 aliyokiandikia chama hicho, akikipa siku tano kujieleza kwa nini kilivunja sheria na kanuni.

Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kwa mara nyingine ametoa siku tano kwa CHADEMA kujieleza kwanini asikichukulie hatua kwa kukiuka sheria na kanuni za maadili ya vyama vya siasa.

Katika barua hiyo ya Jaji Mutungi ya Machi Mosi, 2018 iliyopokelewa CHADEMA Machi 2 inatakita chama hicho kikuu cha upinzani nchini, kujieleza kwa nini kilivunja sheria na kanuni hizo Februari 16, 2018.

Barua hiyo ya Jaji Mutungi inatokana na kutoridhishwa na majibu ya barua yake ya Februari 21 aliyokiandikia chama hicho, akikipa siku tano kujieleza kwanini kilivunja sheria na kanuni hizo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Machi 4, 2018, mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa CHADEMA, John Mrema amesema barua hiyo wameipokea jana na kesho wanatarajia kuijibu.


Chanzo:
 Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search