Tuesday, 13 March 2018

Kakonko: Diwani CHADEMA afunguka Polepole alivyomtumia watu kumshawishi kujiunga na CCM

Tangu juzi natafutwa eti nikubaliane na Ndugu Humphrey Pole pole ili nijiunge na Chama Cha Mapinduzi.
Ndugu huyu alikuja Kakonko,wiki iliyopita na baadae akaenda Dodoma ila aliacha vijana wanaofanya biashara ya kununua madiwani Kakonko na wanazunguka,usiku na mchana wakitafuta madiwani wa upinzani,wamenipigia simu nyingi,nina Audio zao,wanaahidi kukupa stahiki zote,na wanasema wao wanahakikisha unashinda udiwani kwa gharama yoyote ile.

Polepole amerudi Kakonko leo tarehe 11/03/2018 kuangalia vijana wake wamefikia wapi katika manunuzi haya haramu na ya kishetani.

Sijawahi kuona biashara ya watu katika umri wangu,nimeiona sasa,tena safari hii anayetaka kununuliwa ni Mimi, Mungu lehemu taifa lako.
Watawala wamejificha kwenye kivuli cha uwajibikaji na kutangaza elimu bure pasipo madawati,pesa zimetengwa ili kumununua diwani wa Gwarama.

Wanunuaji wetu wanatumia gari ya wagonjwa kukata misere mtaani kutafuta diwani ambae wao wanataka akihame chama kwa Kusema nimekubali MZIKI WA MAGUFULI!!.

Kakonko ina hali mbaya ya Kiuchumi kiasi kwamba madiwani tunadai posho miezi 12 sasa. Tunakopesha vikao,hatunywi maji kwenye vikao,kuna roho zipo zimesubiri uombe maji ya kunywa halafu upewe na sumu ili udiwani ambao ni uwakilishi wa wananchi ukome kwa kukukatiza maisha ili chama kinachoitwa PENDWA kishinde,ushindi wa chama hiki ni mpaka adui afe kama siyo kufanywa kilema kwanza!!

Nimewaambia viongozi wa dini biashara hii kama imefika Gwarama,nao wamesema nisikubali kuuza Uwakilishi huu kwasababu ya kutafuta urahisi wa maisha na chakula.
Na mimi nilishakubali kuongozana na maskini wenzangu.
Naheshimu kura za maskini wenzangu,siwezi uza kura za hawa maskini wenzangu ili Mimi niutwae utajiri kwa kuwadhuru maskini.
Inahitaji roho ya ushetani kukubaliana na biashara hii inayofanywa na chama kinachoongozwa na mtu anayetamba kuwa MCHA MUNGU ambaye wiki chache alipakwa majivu usoni!!

Mungu okoa hili Taifa maana hali ni tete ila watu wanaona kawaida.
Heri wenye moyo safi maana hao watamuona Mungu.

Elia F Michael
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa madiwani kanda ya Magharibi
11/03/2018. IMG_20180311_143504.jpg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search