Thursday, 29 March 2018

Lissu asema kilichompata Mbowe, viongozi Chadema ni maandalizi kuelekea Ikulu

LISSU.jpg ​Dar es Salaam. Siku moja baada ya viongozi sita wa Chadema, akiwamo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kushtakiwa kwa makosa manane na kukosa dhamana, Tundu Lissu amesema kitendo hicho ni maandalizi ya upinzani kuelekea Ikulu.

Akizungumza leo Jumatano Machi 28, 2018 na MCL Digital, mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) aliyeko nchini Ubelgiji kw amatibabu, Lissu amesema kilichowapata viongozi hao hakiwezi kuzima madai ya kudai demokrasia.

Viongozi hao wamelala mahabusu wakikabiliwa na mashtaka manane ikiwamo kufanya uasi, kuhamasisha chuki na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi, Akwilina Akwilini.

Pamoja na Mbowe, viongozi wengine ni katibu mkuu, Dk Vicent Mashinji; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; naibu katibu mkuu (Bara), John Mnyika, naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko.

“Ukandamizaji huu ni maandalizi tu ya kwenda Ikulu. Hawatafanikiwa kuzima moto wa madai ya demokrasia na haki za binadamu,” amesema Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search