Tuesday, 6 March 2018

MBOWE ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI KCMC


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa KCMC akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa, ameruhusiwa.

Ofisa Habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema leo Jumatatu Februari 5, 2018 kuwa Mbowe ameruhusiwa baada ya madaktari kuridhishwa na afya yake iliyorejea katika hali ya kawaida.
Mbowe alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.

Chisseo amesema walimpokea Mbowe jana jioni Machi 4, 2018 akiwa na maumivu makali ya kichwa.

Amesema hali ya Mbowe inaendelea vizuri na amepumzishwa hospitalini hapo.

"Jana jioni tulimpokea Mbowe, taarifa zinaonyesha alikuwa na maumivu ya kichwa. Taarifa za kitabibu zinaonyesha ni uchovu," amesema Chisseo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search