Thursday, 8 March 2018

Mbunge Hussein Bashe afanya mkutano na waandishi wa habari

Mbunge wa Nzega Mjini anaendelea na press conference ili kuelezea zaidi dhamira yake na hatua yake ya kupeleka bungeni hoja binafsi inayohusu hali ya usalama nchini...

Updates.....

"Ili CCM iendelee kuaminika ni lazima ihakikishe inasimama na wananchi na kuhakikisha kuwa matatizo ya wananchi yanapata ufumbuzi" Bashe

"Kwa utafiti wangu mpaka sasa viongozi wa CCM waliokufa kwa matukio ya kihalifu ni zaidi ya 15. upinzani wamefariki wengi, wakina Mawazo na wengine wengi, haya ni matukio yanatokea kwa sababu za kisiasa, tunataka kuona hatua zinachukuliwa" Bashe

"Nakiri kutoa kauli ya wana CCM kujilinda kule Mbweni mwaka jana, lakini ilitokana na Chadema kutushambulia kwenye msafara na katibu mwenezi wetu wa chama wakati tunakwenda kwenye kampeni" Bashe

"Nimewasilisha barua kwa katibu wa wabunge wa CCM Bungeni kuhusu kusudio la hoja yangu, hivyo wanaosema nimekurupuka ana nataka kukichafua chama changu wanapoteza muda" Bashe

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search