Thursday, 29 March 2018

Mbunge Peter Lijuakali: Ubunge wangu angekuwa mtu mwingine angenyoosha mikono juu na kusema, "Jamani ubunge wenu huo"

FB_IMG_1522266532576.jpg
Anaandika Mbunge wa Jimbo la Kilombero Peter Lijuakali
UBUNGE WANGU ANGEKUWA MTU MWINGINE ANGENYOOSHA MIKONO JUU NA KUSEMA, "JAMANI UBUNGE WENU HUO".

Tangu nichaguliwe kuwa mbunge wa jimbo la Kilombero nimeshtakiwa mara tatu. Zote ni kesi za kisiasa tu.

Mara yakwanza aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm, 2015, baada ya kushindwa kwenye masanduku ya kura alikwenda mahakamani kufungua kesi ya kupinga matokeo yaliyonipa ushindi.

Ile kesi ilichukua mwaka mzima, nikashinda kwa kuonekana nilishinda uchaguzi kihalali.

Sikukaa sawa nikabambikiziwa kesi nimefanya fujo siku ya uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, wakanihukumu miezi 6 jela.

Nilikata rufaa na kushinda kwa kuonekana nilihukumiwa kimakosa huku tayari nikiwa nimekaa jela zaidi ya miezi miwili. Nilikaa jela wakati sikuwa na hatia yoyote masikini!

Mara ya tatu ndio hii, sikuwepo Sofi-Malinyi wakati matokeo ya uchaguzi yakitangazwa ajabu nashtakiwa nimechoma moto ofisi ya kijiji!

Lengo ni kuniyumbisha lakini niko imara kwa maombi ya Wanakilombero na kusimamiwa na Mwenyezi Mungu.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search