Tuesday, 27 March 2018

Mhe. Freeman Mbowe na viongozi Wengine waripoti kituo kikuu cha polisi, wawekwa mahabusu

M/kiti wa CHADEMA Taifa,MheFreeman mbowe akiwasili kituo cha Polisi Kati Dar,kuitikia wito wa polisi ikiwa ni muendelezo wa kufanya hivyo kila wanapohitajika, Viongozi wengine waliowasili ni KM Dkt Vicent mashinji ,NKMB John Mnyika (Mb) NKMZ salum mwalimu na Ester Matiko (Mb)

Viongozi 5 wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, wamewekwa mahabusu baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi mapema leo.

Viongozi hao waliitwa kwa ajili ya mahojiano kuhusu tuhuma za kuhamasisha vurugu wakati wa uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la Kinondoni.

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa naye ameunganishwa na viongozi wa chama hicho waliowekwa mahabusu mchana wa leo katika kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam

Viongozi hao watafikishwa Mahakamani kesho kujibu tuhuma za kuendesha maandamano kinyume cha taratibu baada ya kufutiwa dhamana yao kwa maelekezo ya Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar-es-Salaam(ZCO).

mbowe.jpg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search