Thursday, 1 March 2018

MKUU WA MAHJESHI AWATAHADHARISHA WATANZANIA

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewahadharisha Watanzania na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.
Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.
Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo hivyo
Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu wote.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search