Thursday, 15 March 2018

MMILIKI WA MABASI YA SUPER SAMI AKUTWA AMEKUFA MTONI,..INATISHA ANGALIA PICHA


Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah unaodaiwa kukutwa mtoni ukiwa umefungwa kwenye mfuko wa sandarusi na turubai
Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah enzi za uhai wake

 Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Nabata uliopo wilayani Bunda mkoani Mara.

Taarifa kutoka vyanzo vya habari vya Malunde1 blog ni kwamba mwili wa Samson Josiah umekutwa ukielea katika mto huo leo Jumatano Machi 14,2018 majira ya saa 10 jioni

Inaelezwa kuwa mwili huo umekutwa umefungwa katika mfuko wa sandarusi na turubai.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Mara.

Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search