Friday, 23 March 2018

MWALIMU MBARONI KWA KUMKASHFU RAIS MAGUFULI MITANDAONI

Mwalimu wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia.

Aidha amesema kuwa kufutia hali hiyo tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi ili washughulikiwe

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search