Thursday, 1 March 2018

MWANAMUZIKI AHUKUMIWA JELA KWA KUTOA NENO LA UTANI

MWANAMUZIKI maarufu nchini Misri na Jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice, Sherine Abdel Wahab amehukumiwa miezi sita jela kwa kutania juu ya hali ya usafi wa mto Nile baada ya kuwaambia mashabiki wake kuwa kunywa maji ya mto huo kunaweza kumpatia vijidudu ya maradhi.
Sherine alifunguliwa mashitaka mwezi Novemba, baada ya kuonekana video mtandaoni ikimuonesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha “umewahi kunywa maji ya mto Nile?” Akajibu ‘‘Nikinywa maji ya mto Nile nitapata kichocho, kunywa Evian badala yake,” alisikika akitania.
Abdel Wahab baadae aliomba radhi kutokana na tukio hilo akiwa kwenye tamasha lililofanyika huko Jumuia ya falme za kiarabu zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search