Wednesday, 7 March 2018

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Abdul Nondo aliyekuwa anakosoa mwanafunzi Akwilina kuuawa na Polisi, hajulikani alipoju2.jpg 
Abdul Nondo ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania

Kuna taarifa za kutekwa kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania ndugu Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa UDSM. Jana usiku saa sita, kabla ya kupotea hewani alituma text kwa rafiki yake kuwa "I AM AT HIGH RISK". Nondo hakupatikana tena hewani hadi sasa.

Kabla ya kupotea hewani, Nondo alileft magroup yake yote ya whatsapp, jambo lililozua taharuki. Alijaribu kupigiwa simu, hakupokea na hiyo likuwa mida ya saa 5-6 usiku. baadaye akatuma ujumbe kwa rafiki yake kuwa kuwa yuko HATARINI.


Abdul Nondo amekuwa akikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya ndani. Mara ya Mwisho kuongea na Wanahabri, alishinikiza Mwigulu Nchemba kujizulu.

"Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu nafasi yake kwa sababu ameshindwa kulinda haki, usalama wa raia, katika kipindi chake ndiyo matukio mengi makubwa yameshamili. Mhe Mwigulu ni kiongozi wa kisiasa inatakiwa achukue kitu kinaitwa 'individual responsibility' ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kuangalia mienendo ya jeshi la polisi linavyofanya sasa hivi saizi kila siku tunasikia matukio mara huyu kauawa, huyu katekwa hakuna kauli ya jeshi la polisi na hakuna kauli ya moja kwa moja kutoka wa Waziri yaani juzi amesimama anasema naomba jeshi la polisi liangalie upya na kufanjya uchunguzi matukio yanayotokea, Tanzania tumekuwa na uchunguzi mwingi sana ila kujiuzulu kwake kutasaidia" alisema Nondo

Habari zaidi zilizopatikana mchana huu kutoka kwa marafiki zinasema'' ni kweli Abdul Nondo hajulikani alipo mpaka sasa lakini taarifa zilizopo ni kuwa alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa Mtandao wa Wanafunzi kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kuleft magroup ya Whatsapp

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi, kuhusu Abdul ni kweli hajulikani yuko wapi mpaka sasa, hata Wazazi wake(Mama na Baba yake mdogo) hawajui yuko wapi. Viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi wamefika Kituo cha Polisi kilichopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwaajili ya kutoa taarifa za kupotea kwake''
For The English AudienceAbdul Nondo, The Chairperson of Tanzania Student's Network is alleged to be abducted by unknown people.

Before he went missing, he left form all WhatsApp groups, an act that raised suspicions among his friends. After that it is claimed that he sent an SMS to his friend saying "I am at high risk" and his phone has been unreachable since that moment. The Network leaders have already reported the matter to the Police.

There has been a trend of abductions in the country at the moment especially towards Government critics, and most people are connecting this event to several others of the sort.

A few weeks ago, Nondo criticized and blamed the Government for the fatal shooting of Akwilina Akwilin, a female student of NIT who was shot dead during an opposition demonstration in Dar es Salaam and he was quoted vocally asking the Minister of Home Affairs, Dr. Mwigulu Nchemba to resign.

Several people have been abducted/disappeared in recent times including "Roma Mkatoliki" a hiphop artist, 5 religious leaders from Zanzibar, Journalist Salma Said and up to now, Ben Saanane, a popular government critic and Azory Gwanda, a journalist have been missing and all blame is directed towards the Government.
criedit:Jamii forum

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search