Monday, 12 March 2018

Naibu Katibu Mkuu BAVICHA, Getrude Ndibalema ajiuzulu nafasi yake na kubaki mwanachama wa kawaida

Naibu Katibu Mkuu Bavicha, Bibi Gertrude Ndibalema amejiuzulu nafasi yake na kuendelea kuwa mwanachama wa Kawaida. Amechukua uamuzi huo ili apate muda wa kufanya mambo yake mengine nje ya shughuli za Kisiasa.

Kokwenda.jpgDar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Gertrude Ndibalema amejiuzulu wadhifa huo kuanzia jana Machi 11,2018.

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 ametangaza kujiuzulu kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 12,2018 Gertrude amesema, “Ni kweli nimeamua kuachia nafasi yangu ili kutimiza malengo ya shughuli zangu binafsi.”

“Kwa kuwa nakipenda chama changu na kwa taaluma yangu (mawasiliano kwa umma) ili kuepuka mgongano, nimeamua kukaa pembeni ili kutimiza azma yangu na nitabaki kuwa mwanachama,” amesema.

Gertrude ni kiongozi wa pili wa ngazi ya juu Bavicha kujizulu akitanguliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi aliyejiunga na CCM.Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search