Monday, 5 March 2018

Nape: Kubadili ukomo wa madaraka ni ushetani, unafaa kupingwa kwa nguvu zote na vijana

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kuwataka vijana wa kiafrika kuamka na kupinga baadhi ya viongozi wanaotamani kubadili ukomo wao kuwa madarakani kwani wasipofanya hivyo tabia hiyo itazoelekea na kuwa ya kawaida.

Nape ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo ukiwa umeambatana na picha iliyokuwa inawaonesha baadhi ya wabunge wa nchi ya Uganda wakiwa Bungeni wakitaka kupigana.

"Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa. Hii ni zaidi ya kansa", amesema Nape.

Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya kuonekana kwa baadhi ya viongozi Afrika wakibadili vipengele vichache ndani ya Katiba ya nchi yao ili imuwezeshe kukaa madarakani zaidi ya alivyotakiwa kwa mara ya kwanza kuongoza. 

n.PNG

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search