Wednesday, 21 March 2018

Polisi Mwanza wavamia msiba wakihofia viongozi CHADEMA kufanya vikao vya siri. Mjane azimia...

Polisi mwanza.png
Kwa mara nyingine Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limevamia msiba mwingine na kuwafurusha waombolezaji kwa silaha za moto kwa madai kuwa viongozi wa Chadema wanatumia misiba ya wafuasi wao kufanya vikao vya siri vya kisiasa.

Kitendo cha polisi kuvamia msiba huo na kufurusha waombolezaji kimeongeza uchungu kwa familia iliyofikwa na msiba huo, huku mjane wa marehemu akipoteza fahamu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Ahmed Msangi amesema zoezi la kuwafurusha wafuasi wa Chadema wanaotumia misiba kufanya siasa ni endelevu, huku akisifu nguvu ndogo iliyotumika kuwafurusha waombolezaji hao na kudai wakati mwingine watatumia nguvu kubwa ikiwa waombolezaji watajaribu kuzuia polisi kufanya kazi yao.!

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search