Wednesday, 21 March 2018

Rais Magufuli amewateua aliyekuwa IGP, Mangu kuwa Balozi nchini Rwanda na Meja Jenerai Mstaafu, Mumwi Balozi Urusi

Rais John Magufuli kesho Jumatano Machi 21, 2018 atawaapisha mabalozi wateule wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania nchini Rwanda na Russia.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Machi 20, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Mkuu wa Jeshi la Polisi wa zamani, IGP Ernest Mangu ataapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali mstaafu Simon Mumwi kuwa balozi wa Tanzania huko Russia.

Hafla ya kuapishwa kwa mabalozi hao wateule itafanyika Ikulu Dar es Salaam kuanzia saa 5 asubuhi.


57003107-405f-440b-8d33-7cb32b8961c5.jpeg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search