Tuesday, 27 March 2018

Rais Magufuli apokea ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali, 49% pekee ya fedha za maendeleo zimefika chini

Rais Magufuli anapokea ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, kuwa nami.


====

Udhaifu katika usimamizi wa mikataba serikali Kuu
Alieanza kuongea ni mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, Mussa Assad na anaziongelea taasisi za Umma 14 ambazo zimefanya manunuzi na kupokea bidhaa na huduma bila kugaliwa na kamati zinazohusika kinyume na kanuni ya manunuzi ya umma ya mwaka 2013.

Taasisi nane zilikuwa na manunuzi ya vifaa, kazi na huduma vyenye thamani ya bilioni 53 vilivyoagizwa na kununuliwa lakini havikupokelewa. Vimelipwa lakini havikupokelewa.


Mamlaka ya serikali za mitaa:

Kiasi gani cha pesa kilichopangwa kinafika! Serikali za mitaa zinazofika 146 hazikupata kias cha Tshs bilioni 582 amazo ni asilimia 15 ya bajeti yote ya serikali za mitaa, CAG ameomba kiasi kikipangwa kifike ili seriakli za mitaa ziweze kufanya kazi yake kama ilivyopangwa.

Fedha za matumizi ya Maendeleo:
Serikali za mitaa zinazofika 167 hazikupokea Tshs bilioni 532 sawa na asilimia 51 za fedha za maendeleo amazi hazikufika katika serikali za mitaa. CAG nasema zikipangwa fedha za maendeleo na asilimia 51 isipofika, serikali za mitaa zinaata kazi kubwa zaidi ya kutekeleza malengo yake kwa sababu pesa hazikutosha.


Mh Raphael Chegeni anasema;

Anamuhakikishia Mh rais mapato kuzidi kuongezeka, pia anasema wamefanikiwa kukagua kiasi cha shilingi bilioni 885 ambacho ni mapato yasiyotokana na kodi.

Anaongeza kuwa; Mkaguzi amesema mashirika ya umma yanafanya vizuri, wao kama kamati wanataka yafanye vizuri zaidi.

Amelalamikia kitendo cha ofisi ya msajili wa hazina kuwa na watendaji wanaokaimu nafasi zao, na kupendekeza ipate watendaji wenye sifa na wenye uwezo wa kusimamia ofisi hiyo.

Anawashauri wenyeviti wa taasisi za umma wafanye kazi inavyotakiwa na wao wanamuunga mkono mh. Rais

Mh. Hawa Ghasia, Mwenyekiti wa kamati ya bajeti.
Kinachotakiwa ni kuangalia hati zenye mashaka

Ombi lake; walioonekana wamefanya vibaya na hati zenye mashaka washughulikiwe

Anafurahishwa na bajeti ya CAG kuongezwa japo anazidi kumsisitiza mh rais amuwezeshe CAG kufanya ukaguzi kwenye halmashauri.

Anavitaka vyombo vinavyohusika(Plisi na TAKUKURU) kuwachukulia hatua walioiba fedha za umma.

Anaomba mfuko wa mahakama na wenyewe uwezeshwe ili uweze kushughulikia


Mh Dr Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge

Anaanza kumshukuru mh rais kwa kujitolea sana katika kulijenga taifa.

Kama bunge watapata fursa ya kuzipitia hiyo taarifa ya ripoti na kuweza kuishauri na kuisimamia serikali.

Mh Naibu Spika anamshukuru tena CAG na mh rais


Sasa ni jaji mkuu wa Bunge Prof Ibrahim Juma.

Anamuhakikishia Prof. Asad, kuwa wao kama mahakma watawajibika.

Maeneo yanayotajwa ni kesi za kodi kukamilika haraka.

Anamuahidi mh Rais kurejea masuala haya ya kodi na kuweza kutoa ushauri namna ya kubadilisha.


Waziri Mkuu wa JMT
Anaanza kumpongeza mh rais

Taarifa inatoa matumaini na pia inaonyesha mapungufu makubwa waliyonayo.

Anawahakikishia kamati za bunge kuwa ushauri walioutoa serikali itaufanyia kazi.

Anamlizia kwa kumkaribisha mh RaisMh Rais Magufuli.

Anamshukuru CAG kwa ripoti iliyogusa maeneo ambayo itasaidia kudhibiti matumizi yetu.

Anaendelea kusema ripoti wameipokea na watazifanyia kazi.

Mh rais anafurahishwa na improvement ya hati safi

96 mashirika ya umma
90 tamisemi
80 Serikali imeshuka kutokana na vyama vya siasa

Kuna kesi zilizopo mahakamani zenye thamani ya trilioni 4.4 na mpaka sasa hazijakuwa solved.

Jana mh rais aliandikiwa na waziri wa TAMISEMI kuhusu fedha za maendeleo ambapo hawajakubaliana makao makuu yajengwe wapi.

Nimeagiza hizo fedha zirudishwe hazina.

Na viongozi wanaokwamisha ni viongozi wakubwa kabisa.

Halmashauri ya Kigoma Ujiji ina hati chafu. Wakurugenzi wa wilaya hizo wasimamishwe kazi.

Na kwa kuwa mimi ndo huwa nawateua basi wasimamishwe kazi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search