Monday, 26 March 2018

RAIS MAGUFULI AWAOMBA MAASKOFU KUOMBEA KUJENGWA VIWANDA VYA DAWA

Rais Magufuli leo akiwa anapokea magari 181 ya kupokea dawa MSD, amegusia yanayozungumzwa na viongozi wa dini juu ya hali ya usalama, siasa na uchumi hapa nchini

Rais amesema maaskofu wanatakiwa pia kuhubiri kwa wananchi jinsi ya kukuza uzalishaji wa bidhaa hapa nchini kwa kuanzisha viwanda ili kuokoa fedha nyingi zinazotumika kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi

''Tunatenga bilioni 260 kununua dawa lakini ni 6% tu ndio zinanunuliwa ndani. Niwaombe Maaskofu na Wahubiri wengine waliombee hili, wawekezaji na wafanyabiashara wawekeze. Tunaishia kukemea mengine yasiyo na tija kwa Watanzania."

"Kusubiri ni kugumu, tutengeneze njia sasa, Wizara ya Afya kaeni na wafanyabiashara wa ndani muone namna ya kuwawezesha wafungue viwanda vya dawa...tuwakusanye pia mafamasia wetu tuone namna ya kuwawezesha kufungua viwanda, na majeshi yetu pia," Magufuli.Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search