Monday, 12 March 2018

Rais Magufuli: Mimi ni Rais kweli kweli, jiwe. Sitishwi wala sitishiki; azindua kiwanda cha Alizeti mkoani Singida
Rais Magufuli leo hii anazindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti mkoani Singida Mount Meru Millers baada ya kutoka mkoani Geita akiwa anazindua miradi mikubwa ya barabara.

Waziri wa viwanda na biashara Mh Charles Mwijage:Singida ina viwanda 543 lakini kiwanda kikubwa ni kimoja tu.

Wabunge wa Singida: Watahakikisha wanamlinda kwa nguvu zao zote Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hata kuku hawataandamana na chochoko zote zile ndani na nje ya CCM zitadhibitiwa.

=====

Rais Magufuli: Amesema kuwa Waagizaji wa mafuta ghafi kutoka nje wamekuwa wakifanya ushawishi kwa wabunge ili kupunguziwa kodi au kutokulipa kabisa

Kutokana na mchezo huo aliouita kuwa mchafu ameziagiza mamlaka husika kutoka kodi kubwa kwa mafuta ghafi yanayoagizwa

Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa mkoa wa Singida muda mchache kabla ya kukizindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.

"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki mimi jukumu langu ni kwaajili ya watanzania, nikuhakikisha nawavusha watanzania kutoka mahali kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha. Ninajua hiyo ndio itakuwa sadaka yangu kwa watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko mbinguni Mungu atakaponihitaji, akanichague kutokana na mimi nilikuwa kiongozi mzuri hivyo unaweza hata kuongoza Malaika polepole kwasababu ninajua kuna maisha baada ya maisha ya hapa duniani", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "ndio maana nawaomba sana viongozi wa dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tuitangulize Tanzania kwanza, tusitumike".

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Maguli amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa hakuna maandamano yatakayofanyika, hakuna ruhusa ya kuandamana wala sehemu ya kufanyia maandamano

Hata ikitokea watu waandamana chumbani kunguka kitanda, ikitokea mmoja akaumia basi aliyewaita atawajibika

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya

Mwigulu ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatakanywa tawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.

"Njama hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma. Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa. Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana".

Aidha, Waziri Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.

"Ikitokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atakuwa nala kuajibika kwasababu watu wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania", amesisitiza Mwigulu.

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.
For the English AudienceTanzania’s Minister for Home Affairs, Dr. Mwigulu Nchemba has declared today that there won’t be any demonstrations, neither the permission nor the venue to do so.

"I have realized that there is a group consipiring to murder Tanzanians in the said demonstrations and blame it on the Government. I have instructed the IGP to arrest everyone responsible", said the Minister.

He added, "Hon. President, there are many toys like the one who claimed he was abducted a few days ago but got time to change clothes and freshen himself up with perfumes where he was taken. Where do you get such time in the hands of your abductors? These are conspiracies to tarnish our image and as per your instructions we shall not play games."

The Minister finished by warning Tanzanians that even if they demonstrate in their bedrooms and one of them gets injured the one who organized the demonstration will be accountable.

Dr. Nchemba joins the list of politicians who have warned against demonstrations in recent weeks including President Magufuli, Dar es Salaam Regional Commissioner and the Tanzania Police Force.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search