Monday, 19 March 2018

Rais Mstaafu Mkapa, ataka mjadala wa kitaifa kujadili hali ya elimu nchini baada ya shule za Serikali kufanya vibaya

mKAPA.jpg ​

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamini William Mkapa amesema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa

Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu na kumuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula.

Mhe.Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi ama ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana.

Chanzo: EATV

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search