Wednesday, 21 March 2018

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA SHIRIKA LA NYUMBA(NHC) BI BLANDINA NYONI

bla.jpg 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation - NHC) Bi. Blandina Nyoni kuanzia leo tarehe 21 Machi, 2018.

Pia Mhe. Rais Magufuli ameivunja Bodi ya NHC kuanzia leo.

Uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,

IKULU Dar es Salaam

21 Machi, 2018

--------

Bi. Nyoni aliteuliwa kuiongoza Bodi hiyo Februari 25, 2017 baada ya Zakia Meghji kumaliza muda wake.

nyo.jpg 


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search