Wednesday, 21 March 2018

Serikali yafunguka kuhusu kushambuliwa afisa wa Syria, Bw.Halim Al Faouri na kuporwa pesa, simu na gari la Ubalozi

bALOZI.jpg
Baada ya kuwepo kwa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kushambuliwa kwa afisa wa ubalozi wa Syria nchini Tanzania na watu watatu wasiojulikana na kupigwa ikiwa pamoja na kuporwa pesa, simu na gari aliyokuwa akiitumia kwa shughuli za ubalozi. 

Afisa huyo baada ya kushambuliwa aliporwa gari, simu pamoja na fedha kiasi cha Euro 9300 sawa na zaidi ya Milioni 25 za Kitanzania.

Kufuatia taarifa hizo Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abasi amefunguka na kukiri kupata taarifa hizo na kudai kuwa serikali inafuatilia suala hilo na itatoa taarifa kamili kuhusu jambo hilo.

"Umma unaarifiwa kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za Afisa Ubalozi wa Syria nchini kushambuliwa, kuporwa. Taarifa kamili itatolewa" alisema Abasi

Aidha katika taarifa za awali zinadai kuwa afisa huyo amelazwa katika hospitali ya Agha Khan akipatiwa matibabu kufuatia shambulio hilo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search