Monday, 5 March 2018

Tanzania imeendelea kung'ara, imepanda juu zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi

 1. => Hivi karibuni nilifanya ziara hapa Dodoma kwa lengo la kuona utendaji kazi na kujua baadhi changamoto mbalimbali, nawaomba Wanahabari, tuendelee kufanya kazi zetu kwa weledi mkubwa bila kukiuka misingi ya Taaluma.

  => Kufikia Februari 2018 Serikali imeendelea kutekeleza ahadi zake mbalimbali kwa wananchi kwa lengo la kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania.

  => Tanzania imeendelea kung'ara kimataifa ambapo Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Transparency International iitwayo Curruption Perception Index 2017 imeonesha nchi yetu imepanda kwenda nafasi juu zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

  => Serikali pamoja na miradi mingine mbalimbali nchini inatekeleza miradi miwili mikibwa ya uzalishaji wa umeme wa gesi ambayo ni K- 1 extension( Megawati 185) na Kinyerezi II wa megawati 240.

  => Mradi wa Kinyerezi II ambao utazalisha megawati 240 unatekelezwa kwa 15% fedha za Serikali (ambazo zimeshatolewa) na 85% ni mkopo, Mpaka sasa Mradi umefikia 90% kukamilika ambapo kufikia Februari 2018 jumla ya megawati 111.88 zimeshaingizwa katika gridi ya Taifa.

  => Katika taarifa ya Januari, 2018 tulieleza ununuzi wa mabehewa ya kisasa ya abiria na ya mizigo takribani 1,590 na vichwa takribani 25 na mitambo mengine.

  => Takribani Kampuni 54 zimejitokeza ambapo kati ya hizo 35 zimerejesha nyaraka za zabuni kutoka mataifa mbalimbali na tathimini inaendelea.

  => Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa maziwa makuu ya nchi yetu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria.

  => Meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na mizigo tani 400 Ziwa Victoria, mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwaka huu.

  => Julai mwaka huu nchi yetu itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo Boeing Dreamliner hivyo ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa/Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi nchini.

  => Ujenzi wa Terminal III Dar es Salaam uko zaidi ya asilimia 50, Jengo la Abiria Uwanja wa Kimataifa wa Songwe lipo asilimia 57.

  => Viwanja vingine zaidi ya 10 ujenzi au ukarabati unandelea katika maeneo ya Kigoma, Tabora, Mwanza Geita, Shinyanga, Sumbawanga, Mtwara, Musoma n.k.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search