Thursday, 8 March 2018

Ukaguzi vyeti feki sasa kutua elimu ya juu


Serikali imesema inaandaa utaratibu wa kuhakiki vyeti vya taaluma vinavyotolewa na vyuo vya elimu ya juu vya ndani na nje ya nchi.

Wakati hayo yakielezwa, watumishi wa umma 14,409 wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi huku 1,907 wakiwa hawajawasilisha vyeti kwa ajili ya kuhakikiwa licha ya Serikali kutoa muda wa kutosha kwa watumishi hao kuwasilisha vyeti vyao Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa ajili ya uhakiki...

Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu Utumishi, Dk Laurean Ndumbaro wakati akipokea taarifa ya sita na ya mwisho ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search