Wednesday, 14 March 2018

Uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa reli ya 'standard Gauge' kutoka Morogoro-Makutupora, Dodoma. Magufuli alonga


Kutoka Ihumwa, nje kidogo ya mji wa Dodoma, Rais Magufuli leo anaweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kiwango cha standard gauge ambao itaanzia Morogoro ikiipokea reli inayojengwa sasa kutoka Dar es Salaam na itaishia Makutopora, Dodoma.

Makubaliano yalifanyika Septemba 26, 2017 kati ya RAHCO na kampuni ya kituruki ya Yapi Merkezi baada ya wakandarasi 15 kujitokeza wakati wa zabuni. Kilometa 336 za njia kuu na 86 za kupishana treni kujengwa. Mkandarasi pia atakuwa na jukumu la kujenga njia za umeme na ujenzi utaisha baada ya miezi 36.

Fuatana nami kukujuza yanayojiri Ihumwa mjini Dodoma.


==========

Anaeongea kwa sasa ni Kadogosa na anasema ndio reli pekee Afrika inayoweza kutumika kilomita 160/saa, amemshukuru Rais na serikali yake kwa shirika la reli kuliweka pamoja na sasa linaitwa TRC na anamshukuru kumteua mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo na ameahidi kulitumikia kwa uadilifu.

Anasema miaka mia itakapopita na atakapokumbukwa, waswahili wanasema kwenye msafara wa mamba, Kenge hawakosekani lakini ikumbukwe kenge wema wazuri waliolisaidia taifa.

=========

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde

Anasema reli hiyo itakuza uchumi eneo la Dodoma, anasema Ihumwa ndio wazalishaji wa mchicha mwingi unaotumika soko la Kariakoo na reli ikikamilika mkulima anaweza kutoka na mchicha wake saa moja asubuhi na saa nne atakuwa Kariakoo, saa tano akaenda Mbagala kusalimia na saa sita akapanda treni, saa tisa atakuwa tayari Dodoma, anasisitiza hayo ni maendeleo makubwa sana.
=========

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa

Anamshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa muono wake wa kuona mambo muhimu na taifa ni shahidi kwamba shirika la reli lilishapoteza uwezo wake, amefufua shirika lenyewe lakini pia amekuwa na uchungu na taifa pia kusikia kilio cha watanzania.

Amesema reli hio aliishuhudia Uturuki na Uingereza na kuamua ijengwe Tanzania, anasema sasa anafufua shirika la ndege, bandari na kufufua huduma za jamii kuanzia chini kwa muono wake mkali wa mbali. Anasema jukumu la watanzania na wao wasaidizi wake ni kuona ilani ya CCM inatekelezwa.

Ametoa wito kwa watanzania, kuwa watulivu na kusubiri utekelezaji na kushiriki katika juhudi hizo. Anasema reli ni fursa kwa wote watakaopitiwa na reli hio kuanzia Dar mpaka Mwanza.

Anasema kila mmoja ajitoe kufanya kazi, anasema Tanzania imefikia hatua ya kutolewa mfano na watu waendelee kumuunga mkono na kumuombea Rais magufuli. Kulinda nchi na miondombinu yake.

Amesema watu waachane na hamasa ambazo hazina tija kwao na wao kama Wasaidizi wake hawataruhusu mwanya wowote.
===========

Anaeongea sasa ni Rais John Magufuli

Rais Magufuli: Ihumwa niikuwa napita barabarani, sikujua kama ni mji mkubwa kiasi hiki, kwa kweli wananchi wa Ihumwa, kwa sherehe na baraka hii ya leo naahidi kutengeneza barabara ya lami kutoka hapa mpaka pale njia panda na waziri huyuhuyu wa ujenzi aanze kufanya mipango.

Barabara itandikwe, wananchi wa hapa waweze kufaidi matunda ya maendeleo ya kweli ya Tanzania ili pia treni itakapopita hapa wafanye biashara na watani zangu wagogo, fisi zao zipite kwenye lami.

Moja ya changamoto kubwa bara la Afrika ni kukosekana kwa miondombinu imara na gharama za usafiri kuwa kubwa kuliko sehemu nyingine duniani. Bei ya kusafirisha kontena la futi 20 ndani ya nchi za Afrika mashariki kwa kilomita zisizozidi 1500 ni dola 5,000 bei iliyo sawa na kulisafirisha kutoka China mpaka Tanzania umbali wa kilomita 9,000.

Ujenzi wa reli utatoa ajira na itasaidia kupunguza tatizo la ajira na uharifu wa mazingira kwani itatumia umeme ambao hautoi gesi ya ukaa kwa wingi. Tanzania tuna bahati kwa sababu ya ukubwa wa nchi yetu.

Hivi sasa Tanzania tumefikia idadi ya watu milioni 55, wapo waliosema kwanini milioni 55, tunazaana mno. Mimi nasema tuzaane zaidi, nchi ya Uchina ina watu bilioni 1.3 na ndio maana Uchina uchumi wake sasa hivi uko juu. Lakini mnapokuwa wengi mnakuwa na sauti kwenye block mlizonazo, sisi tupo kwenye East Africa community, tuko milioni 55, idadi ya watu wetu ni sauti tosha.

Kinacotakiwa ni sisi watanzania tuchape kazi, swala si kuwa wengi, namna gani hao watanzania wengi wanashiriki kuleta maendeleo ya nchi yao. Denmark ina watu milioni 5 lakini kwa sababu ya uchapakazi wao wamekuwa wakitoa msaada kwa nchi yenye watu wengi kama Tanzania.

Kwa hio tusiogope kuwa wengi, tukubali kuwa wengi lakini wengi wanaochapa kazi. Hata kama tungekuwa milioni moja lakini hatufanyi kazi tungelia tu njaa.

Siku za nyuma hii reli tuliibinafsisha kwa watu fulani, hakuna ilichofanya na ilikaa na hii reli kwa miaka, tumeamua kujenga wenyewe na waturuki tumewaajiri sisi wenyewe na watanzania popote mlio mjisifu kwa kujenga reli hii, zinakopa na kupewa masharti magumu, tunajenga kwa gharama ndogo kuliko walivyotegemea na asilimia 100 zimetokana na fedha za watanzania. Advance kashapewa zaidi ya biioni 500, sisi ndio mabosi.

Niwaombe TRA, muangalie kodi zenu mnazozitoza, inawezekana zingine ni kubwa mno kuliko miradi wanayoitekeleza wananchi, badala ya kuwa motisha kwa walipa kodi, inakuwa kero kwa walipa kodi na badala yake wanabuni mbinu za kukwepa kulipa kodi wakati wangeelimisha vizuri wangeweza kulipa kodi kwa hiyo TRA mjipange vizuri.

Tulizungumzia kodi za nyumba lakini mmeenda mmetoza mpaka laki sita wakati tuliwaambia mpige flat rate ambayo ingekuwa motisha.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search