Monday, 12 March 2018

WATU KUMI NA SITA WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUPIGWA NA RADI

Watu 16 Wapoteza Maisha Baada ya Kupigwa na Radi
Watu 16 wamepoteza maisha nchini Rwanda baada ya kupigwa na radi wakiwa kanisani katika wilaya ya Nyaruguru iliyo Kusini mwa nchi hiyo.


Watu wote 140 waliokuwa katika kanisa hilo walipelekwa hospitali, lakini wengi waliruhusiwa kurudi nyumbani, isipokuwa watatu ambao bado wako katika hali mahututi.

Meya wa wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois, amesema kuwa siku moja kabla, Radi nyingine ilikuwa imepiga kundi la wanafunzi 18 katika wilaya hiyo, na kuuwa mmoja wao. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search