Wednesday, 21 March 2018

Waziri Mwakyembe amshukia Diamond. Asema umarufu utamgharimu, hawezi bishana na Shonza na atapotea kubishana na serikali

FB_IMG_1521606740815.jpg
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi ni maarufu kiasi gani."

"Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "Si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo."

Chanzo: DAR24

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search