Wednesday, 28 March 2018

ZARI THE BOSS LADY ATUA BONGO-HAYA NDIO ALIYOYASEMA BAADA YA KUTUA

Mpenzi wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan maarufu Zari The Boss Lady ametua nchini Tanzania kwa ajili ya kusaini mkataba wa ubalozi wa kampuni ya Kedz Tanzania inayojihusisha na utengenezaji wa pampasi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumatano Machi 28, 2018 katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, Zari ambaye ni mama wa watoto watano amesema anashukuru kupata mkataba na kampuni hiyo.

Hata hivyo, kiu ya wanahabari ilikuwa kusikia akizungumzia uhusiano wake uliovunjika lakini alikwepa swali hilo akidai kuwa siyo  kilichomleta.

“Unajua hii ni kazi na haihusiani kabisa na masuala ya familia, hivyo nisingependa kulizungumzia hilo leo,” alifafanua.

Zari alitangaza kuachana na mwanamuziki Diamond Platnumz Februari 14, 2018 kupitia mtandao wa Instagram.

Wiki mbili baadaye akihojiwa na Kituo cha BBC Swahili, Zari amesema ameamua kuachana na Diamond kutokana na sababu mbalimbali moja ikiwa ni kushikana hadharani na mwigizaji Wema Sepetu.

Na Nasra Abdallah, Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search