Saturday, 7 April 2018

ALIYEGUNDUA TANZANITE AJAZWA MAHELA NA RAIS MAGUFULI

Rais John Magufuli amesema Serikali inampa Sh100 milioni Mzee Jumanne Ngoma aliyegundua madini ya Tanzanite.Rais Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 6 wakati wa uzinduzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara leo.


“Watu hawa hawatambuliwi, tazama mzee huyu, ndiye aliyegundua madini haya, leo tusingekuwapo hapa kama asingekuwa huyu mzee. Tazama sasa amepooza mguu wake,” amesema.


Amesema mzee huyo hakutakiwa kuketi katika viti vya nyuma wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa ukuta wa mgodi huo.


Baada ya Rais Magufuli kumuulizia Mzee Ngoma, aliletwa kuketi mbele, akiwa ameshikiliwa kutokana na miguu yake kupooza.


Rais Magufuli amesema fedha hizo zimsaidie katika matibabu yake na katika mahitaji yake mengine.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search