Saturday, 7 April 2018

ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUMEZA MSWAKI

Mtu mmoja nchini Kenya amefanyiwa upasuaji wa kisasa wa kutoa mswaki, aliokuwa ameumeza kwa bahati mbaya wakati akisafisha kinywa.

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la David Charo mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Ganze Kaunti ya Kilifi, alimeza mswaki wakati akisafisha kinywa kujiandaa kunywa chai, tukio lililomsababishia ahisi kama ndio utakuwa mwisho wa uhai wake.

“Nilikuwa najitayarisha kupiga mswaki ndio nikunywe chai halafu nianze safari yangu ya kuja Mombasa. Kupiga mswaki hivi, kwa bahati mbaya ule mswaki ukateleza na ukaingia ndani”, amesema David.

Hata hivyo madaktari wa hospitali kuu ya Coast walifanikiwa kuutoa mswaki huo kwa njia ya kisasa bila kumfanyia upasuaji, na kuokoa maisha yakje.

Imeelezwa kwamba iwapo madaktari hao wangeshindwa kuutoa kwa njia hiyo, wangelazimika kumpasua tumbo ii kuutoa mswaki ambao tayari ulikuwa umeanza kumletea madhara kiafya.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search