Saturday, 7 April 2018

Askofu Mkuu Zachary Kakobe aitwa Uhamiaji Jumatatu 9.4.2018 kuhojiwa juu ya uraia wake

Image result for zakaria kakobe
Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar-Es-Salaam, imemwandikia barua Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, kumwita kwa ajili ya mahojiano. 

Barua hiyo yenye Kumbukumbu Na. BA: 120/231/02/82 ya tarehe 5.4.2018, imemtaka Askofu Kakobe kufika katika ofisi hiyo, Jumatatu 9.4.2018 saa 4 asubuhi, na kuonana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam, ili kuhojiwa juu ya uraia wake. 

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Askofu Kakobe amethibitisha kupokea barua hiyo, na kusema kifupi tu kwamba, atakwenda kwenye mahojiano hayo. 

Tukio hili linakuja baada ya sekeseke kati ya Askofu huyo na TRA, kuhitimishwa tarehe 20.2.2018, siku ambayo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alipotoa taarifa kwa umma juu ya uchunguzi wao; na baadaye kusema mjadala huo umefungwa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search