Thursday, 19 April 2018

HII NDIO SABAU KUU ILIYOMFANYA ALI KIBA KUFUNGA NDOA NA MREMBO WA KENYA

STAA wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba‘ amefunguka na kusema kwamba, yeye alinusa tu na akajikuta amempenda binti mrembo Amina Khaleef kutoka Mombasa ambaye leo, Aprili 19, 2018, amefunga naye pingu za maisha.

 “Wanasemaga macho hayana pazia na moyo hauna macho, lakini mimi moyo wangu umenusa tu mpaka huku, sijaweza kuona lakini moyo wenyewe ndiyo umependa, nipo Tanzania, ningeonaje huku Kenya? Moyo ndiyo umependa.
“Nimejiona nimetimiza umri, ni wakati wangu kuwa na mke, maisha ndiyo haya haya kinachotakiwa ni kupigana nayo ili uweze kuishi vizuri,” alisema Kiba.

Kiba na Amina wamefunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa leo Asubuhi ambapo tukio hilo limeshuhudiwa pia na ndugu na marafiki zake wa karibu.Aidha, Kiba amesema ameamua kufunga ndoa yake siku ya leo kwani siku kama hii ndiyo wazazi wake walifunga ndoa yao miaka kadhaa iliyopita. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search