Tuesday, 24 April 2018

HIVI NDIVYO MASOGANGE ALIVYOPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE

Msanii anayepamba video za muziki (video queen) Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia. 

Akithibitisha taarifa ya kifo hicho daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu  leo jioni Ijumaa Aprili 20,2018, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake, Reuben Simwanzaamesema taarifa za kifo chake amezipata kupitia dada yake, saa chache zilizopita.

Kwa maelezo ya Simwanza, dada wa Masogange, Emma Gerald, ndiye aliyetoa taarifa hizo baada tu ya kutoka kumuona alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria huyo ambaye amedai yeye si msemaji zaidi, kuhusu nini chanzo cha kifo chake, alidai mara ya mwisho waliwasiliana naye siku mbili zilizopita kwa ujumbe wa simu ya mkononi.

“Unajua kuumwa kweli alikuwa anaumwa, kipindi cha kesi yake magonjwa ya hapa na pale ikiwamo presha, si unajua tena mambo ya kesi hayana mwenyewe, lakini baada ya kwisha tulikuwa tunataniana kwamba sasa nina imani utakuwa powa kwani kila kitu kipo sawa,”amesema Simwanza.

Hata hivyo amesema yupo njiani kuelekea hospitali kwa kuwa hakuweza kupata maelezo zaidi kutoka kwa dada yake huyo ambaye amemsikia akiwa analia tu.

Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017.


Leo Aprili 22, 2018 mwili wa Agnes Gerald Masogange unaagwa katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam, na kisha kusafirishwa kwenda kwao Mbeya kwa ajili ya mazishi.

Masogange alifariki dunia Ijumaa Aprili 20, 2018 saa 10 jioni kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya ‘pneumonia.‘Mwili wa Agnes Gerald ‘Masogange” tayari umewasili nyumbani kwao eneo la Utengule-Mbalizi mkoani Mbeya.

Safari ya mwisho duniani ya aliyekuwa msaani maarufu aliyekuwa akipamba video za wanamuziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald 'Masogange' imehitimishwa jana saa tisa alasiri bada ya kuhifadhiwa kwenye nyumba ya milele nyumbani kwa wazazi wake Utengule – Mbalizi mkoani Mbeya.


Maelfu ya waombolezaji kutoka Dar es salaam na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya walijitokeza wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla.


Akitoa salamu za rambirambi kutoka serikalini, Makalla amesema hakuna mtu anayejiandaa wala aliye tayari kwa ajili ya kifo, hivyo kifo cha Masongange ni kilelezo kwamba binadamu wote hapa duniani ni wasafiri.


‘Kifo cha Masogange kitukumbushe kwamba sote tutakufa, nimefurahi namna wasanii mlivyojipanga bila kujali bifu na tofauti zenu, katika hili mmekuwa pamoja,” amesema Makalla.


“Nilikuwa nafuatilia tangu msiba huu ulipotokea, mlikuwa pamoja na kwa mshikamano na sisi Serikali tunawapa pongezi sana.”


Makalla amewapongeza wananchi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na hiyo inaonyesha ndio utamaduni wa Mtanzania kushirikiana katika matatizo.


Akimshukuru Makalla kwa niaba ya wasanii wenzake, mwenyekiti wa wasanii hao, Steve Nyerere amesema, “hili ni pigo kwetu wasanii. Na sisi kama wasanii tumekubaliana kiasi tulichojichanga, kiasi fulani kitatumika kumlipia ada ya mwaka mmoja mtoto wa marehemu ambaye yupo darasa la saba lakini pia kumlipia bima ya afya endelevu.”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search