Thursday, 19 April 2018

MANARA AFUNGUKA NDOTO ZAKE ZA KUWA RAIS WA TANZANIA SIKU MOJA


Afisa Habari wa timu ya soka ya Simba Haji S. Manara, amesema kwamba anaamini kuwa siku moja ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania itakuja timia, kwani ndio tamanio lake la siku nyingi.

Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Haji Manara amesema yeye kama mwanasiasa upande wa pili, ndoto yake kubwa ni kuja kuwa Rais wa nchi baada ya kuzichanga.

“Iko siku mungu akinipa majaliwa, nikazichanga karata zangu, nitakuja kuwa rais, ndiyo ndoto yangu, na ndio ndoto za wanasiasa wote duniani, unaona bunge lile!? kama kuna mwanasiasa ambaye hana ndoto ya kuwa Rais hawafiki watano, mwanasiasa yoyote ukishaingia, hizo ndio ndoto kuja kushika wadhifa wa juu, kama huna ndoto wewe hufai kuishi”, amesema Manara.

Kauli hiyo ya Manara sio mara ya kwanza kusikika akiitamka, huku akisistiza kwamba kwa kuwa yeye ni mwanasiasa mzuri na mkweli, pia ni kada wa CCM, anaamini atakuja kushika wadhifa huo mkubwa kwenye nchi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search