Thursday, 19 April 2018

MASHINDANO YA MBIO ZA KUBEBA WANAWAKE YAZUA GUMZO MTANDAONI


Mshindi wa mchuano wa kubeba mke

Haya ni mashindano ya 11 ya mbio za kubebana nchini Uingereza.

Chris Hepworth, akiwa amembeba Tanisha Prince kutoka West Drayton, London, alikimbia na kuibuka mshindi wa mbio za umbali wa mita 380.

Waandaaji wa michuano hiyo wanasema zoezi hilo lilianza mwezi June mwaka 793 AD.Michuano inahusisha umbali wa mita 380 zenye vikwazo kukiwa na miinuko na miteremko

Washindani walikimbia umbali wa mita 15 kupandisha kwenye mwinuko na kushuka ambapo wameeleza kuwa ni kazi ngumu.

Washindani si lazima wawe na ndoa lakini angalau wawe marafiki.Chris Hepworth, alimbeba Tanisha Prince, aliibuka mshindi

Sheria inasema wenza wawe na zaidi ya miaka 18 na uzito wa kilo 50 na kuna adhabu ikiwa utamuangusha mwenza wako, ikiwa uzito ni chini ya kilo 50 aliyembeba analazimika kubeba furushi lenye vikopo ili kuongezea uzito.

Mshindi anasema kupanda mlima ilikuwa rahisi kuliko kuteremka.

Washindi wataenda kwenye michuano ya dunia mwezi Julai nchini Finland

Bwana Hepworth ana matumaini ya kushinda.Watu takriban 50 walishiriki

Waandaaji walitoa tahadhari wakisema kuwa ''kumbeba mke kunaweza kuwa jambo la hatari, kunakoweza kusababisha majeraha kama ya uti wa mgongo, kuvunjika miguu na mikono, majeraha usoni, kwenye fuvu la kichwa na hata kifo."Ben and Hannah Brackenbury waliingia kwenye michuano hiyo wakiadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao

Ben na Hanna Brackenbury waliingia kwenye mashindano hayo kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya ndoa yao

Wenza hao wamesema walikuwa wakifanya mazoezi kwenye bustani na kwenye mvua wakijiandaa na michuano.Mitindo mbalimbali ya kubebana ilishuhudiwa

Mshindi alipata pipa lenye bia anayeshika nafasi ya mwisho anapatiwa tambi na chakula cha Mbwa.Washindi watakwenda kushiriki michuano ya dunia nchini FinlandAina hii ya ubebaji imeelezwa iliwafanya wakimbie kwa kasiMichuano ya dunia itafanyika mwezi Julai

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search