Tuesday, 24 April 2018

Mchumba mpya wa Zuma alazimishwa kujiuzulu ajira yake

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Mwanamke ambaye anatarajiwa kuwa mke wa saba wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini,Jacob Zuma amelazimishwa kujiuzulu ajira yake ya ukuu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali na chombo cha habari cha nchini humo.
Nonkanyiso Conco ambaye ana mahusiano ya kimapenzi na bwana Zuma ambaye amemzidi umri wa miaka 52. wakati huo yuko kwenye asasi inayohamasisha kampeni ya kuwawezesha mabinti wadogo katika maisha yao ya kila siku na kuacha kuwategemea wanaume wenye umri mkubwa.
Bi.Conco mwenye miaka 24 amejifungua mtoto wa Zuma katika hospitali ya binafsi iliyoko mjini Durban.
Zuma kwa sasa ana umri wa miaka 76,ana wake wanne na mwingine mmoja waliachana na mke wa sita alijiua mwaka 200 pamoja na watoto ishirini.
Nonkanyiso ConcoHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionNonkanyiso Conco,(24)mchumba mpya wa Rais Zuma
Conco analazimika kujiuzulu cheo chake akiwa ni afisa mawasiliano wa kampeni ya kukabaliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wadogo, unyanyasaji wa kijinsia na ujauzito kwa watoto wadogo.
Mpaka sasa Bi Conso hajazungumza chochote kuhusiana na tuhuma zinazomkabili lakini amewasilisha barua ya kujiuzulu kazi katika shirika analofanyika kazi,Daily Maverick limeripoti.
Habari za mahusiano ya Jacob Zuma na Bi Nonkanyiso Conco zilizagaa sana tangu siku ya ijumaa iliyopita

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search