Friday, 20 April 2018

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali(CAG) mbele ya Rais Magufuli akanusha TZS 1.5T kuibwa wala kupotea

 Image result for profesa mussa assad
Majaji wapya walioapishwa mbali ya kuhimizwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, wametakiwa kuzisoma na kuzitafsiri vyema sheria kwani kama watafanya vinginevyo wanaweza kuipoteza nchi.

Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewaambia majaji hao leo Ijumaa Aprili 20 Ikulu kuwa kazi waliyopewa inahitaji umakini na uadilifu.

“Someni sheria na kuzitafsiri vizuri… Mahakama ndiyo chombo pekee kinachotafsiri sheria na kama mtatafsiri vibaya mnaweza kuipoteza nchi,” amesema jaji huyo wakati akitoa nasaha zake baada ya majaji hao wapya kuapishwa na Rais John Magufuli.

Alisisitiza kuwa katika utendaji wa kazi kumekuwa na mgawanyiko wa majukumu wakati Bunge likitunga sheria, Serikali kazi yake kubwa ni kupendekeza sheria hizo.

“Mahakama ndiyo inayotoa tafsiri hivyo ili kuifanya vyema kazi hiyo lazima mtapaswa kusoma sana na someni kwa makini maana kile mnachokiamua nyinyi ndiyo mwongozo wa mwisho mpaka pale Bunge litakapoamua kutunga sheria nyingine,” amesema.

Kuhusu kuishi kwa uadilifu kamishna huyo aliwataka majaji hao kujichunguza mienendo mibovu itakayoweza kuwaondoelea heshima kwa jamii

“Chagueni vyema marafiki zenu ikiwezekana achaneni na wale wanaoonekana kutokuwa wema… na ikiwezekana ukitoka zao kazini nenda nyumbani na siku kama ya leo Ijumaa nenda msikitini kwa wale Waislamu na wale Wakristo nendeni kanisani Jumapili … mnaweza kwenda pia kwenye burudani lakini angalieni burudani mnazokwenda,” amesema.

Rais Magufuli leo amewaapisha majaji wapya kumi, wakili mkuu wa serikali na naibu wake na naibu mkurugenzi wa mashtaka.

Sherehe za kuwaapisha majaji hao zinafanyika Ikulu na zinahudhuriwa na wageni mbalimbali akiwamo Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma.


Rais Magufuli akiwa Ikulu katika hafla hiyo ya kuwaapisha majaji 10 anasema aliposikia kwenye mitandao kuwa Serikali inatuhumiwa kuiba/kupoteza kiasi cha Trilioni 1.5 alimpigia simu CAG kumuuliza kwanini alimficha kuhusu wizi wa kiasi hicho cha fedha alipomsomea Ripoti hiyo Ikulu ili awafukuze wahusika?

Anasema alimwambia CAG kuwa amepitia ripoti yake yote lakini hakuona ilipoibiwa Shilingi trilioni 1.5, CAG akamjibu Rais kuwa hakuna hela iliyoibiwa. Rais akasema ni kawaida ya watu kuandika uwongo kwenye mitandao na kuwaaminisha watu kwa sababu wana uhuru.

Rais anasisitiza angemfukuza mhusika hata angekuwa Waziri siku hiyohiyo kama angeona upotevu wa kiasi hicho cha fedha.

Rais anamuuliza CAG ukumbini hapo na anajibu " Hakuna kitu kama hiko Mheshimiwa Rais". Pia anamuuliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha naye anasimama na kusema " Hakuna kitu kama hicho"

Rais anasema DPP, Solicitor General, Deputy DPP na majaji washughulikie kesi kama hiyo haraka.

Rais amewataka majaji kutafuta njia ya kuwashaghulikia watu wanaojifanya ni wasemaji wao hasa ambao wanapigania maslahi yao(Tanganyika Law Society) kwani wana lengo la kuwachonganisha naye.

"Mnisaidie tu kwa hawa wanaojituma au mnawatuma kuwa wasemaji wenu kwa sababu wananichonganisha na ninyi. Kwa sababu nashindwa kutofautisha wanajituma au mnawatuma. Na kama wanajituma ninyi ni wanasheria tumieni uwezo wenu"

Rais Magufuli aliongeza pia kuwa Watanzania tunaamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii na hiyo inatokana na kutokudhibiti mitandao hiyo. "Sidhani kama ukienda kwenye nchi kama China kama wana 'Google' na 'WhatsApp' kama hizi za kwetu"

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search