Thursday, 19 April 2018

Mlipuaji wa majengo pacha akamatwa

syria al qaeda capture
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionmajengo pacha baada ya kushambuliwa
Wanamgambo wa Kikurdi wanaofanya kazi ya kulinda amani kaskazini mwa Syria wanasema kuwa wamemkamata mtu mmoja mzaliwa wa Syria mwenye uraia wa taifa la Ujerumani ambaye anashukiwa kuwasaidia wanamgambo wa al-Qaeda kupanga mashambulizi ya September kumi na moja nchini Marekani mwaka 2001
Msemaji wa vikosi vya Kikurd ameeleza kuwa Mohammed Haydar Zammar amekuwa akifanyiwa mahojiano tangu alipokamatwa.
Zammar anashutumiwa kuwa ndiye kielelezo muhimu katika shambulizi la uwanja wa Hamburg katika jela nchini Ujerumani miaka ya 1990 wakati Mohammed Atta na wengine walipopewa kazi maalumu kisha kufundishwa kazi ya urubani na hatimaye kuruka na kuzielekeza ndege zao katika jengo pacha la kibiashara la World Trade Center na Pentagon.
Zammar alikamtwa pia nchini Morocco mwaka 2001 na akapeleka Syria lakini serikali ya Damascus ilimuachilia huru baada ya kubadilishana na mfungwa mwenye msimamo mkali

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search