Sunday, 8 April 2018

MOURINHO ATOA TAMKO HILI KUHUSU UNITED

Baada ya kuitwanga Manchester City kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England jana Jumamosi, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema timu yake inastahili kupewa heshima.

United ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 kabla ya kusawazisha na kuongeza jingine ambalo lilidumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo.

Kutokana na matokeo hayo ya ugenini, Mourinho amesema kuwa hakika wachezaji wake walipambana wakiwa ugenini kwa kupindua matokeo baada ya kuwa nyuma kwa bao hizo mbili.

"Nadhani tunastahili kupewa heshima, wachezaji wako vizuri nami niko vizuri kuliko watu wanavyofikiria" alisema Mourinho.

Katika mchezo huo, Manchester City ilijipatia mabao yake kupitia Vincent Kompany na Gundogan huku United wakifunga kupitia Pogba aliyetia kambani mabao mawili na jingine likifungwa na Smalling.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search