Sunday, 8 April 2018

Msimamo wa Rais Magufuli Kuhusu Serikali Kugawa Ng'ombe Longido

"Nimewaita Wabunge wa Arusha hapa waje waeleze shida zao. Shida hizo nimezipokea, lakini ni shida moja tu nataka niijibu hapa, ile ya kugawa ng'ombe. Sigawi Ng'ombe Mimi

Ninafahamu Mzee wangu Kikwete alienda kuwagawia ng'ombe kule Longido. Hilo Mimi siliwezi!

Tukianza na utaratibu huu; Ng'ombe wanakufa halafu Serikali inagawa, Pamba zikikauka Serikali inagawa, Korosho zikiharibika Serikali inagawa, hilo Mimi siliwezi nataka nizungumze wazi

Kwahiyo sitopeleka Ng'ombe Longido nataka niwaeleze hivyo. Zilizogawiwa wakati ule ni hizo hizo. Sijawahi kuahidi kugawa ng'ombe. Huyo ndio Magufuli!"

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search