Thursday, 19 April 2018

MSUKUMA-WENYE MAKOSA MADOGO WAPEWE ADHABU NDOGO ILI KUPUNGUZA MSONAMANO MAGEREZANI

Msukuma: Mlisema Waandamane Mbebe Majeneza 200Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma, amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, kupeleka bungeni muswada  kubadilisha sheria ili makosa ambayo hayastahili mtu kufungwa apewe adhabu ndogo ili kuondoa msongamano katika magereza.

Pia mbunge huyo aliwataka baadhi ya wabunge waache kupiga kelele bungeni juu ya matukio ya watu kupotea na kutekwa, badala yake waviache vyombo vya sheria na vya usalama vifanye kazi yake.Hayo ameyasema Bungeni wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na Sheria jana, Aprili 18, 2018.“Tuna shida sana na majengo ya mahakama huku kwenye vijiji vyetu Geita ambako tunategemea watu wanakwenda kutendewa haki huko, lakini mahakama ni chache na zilizopo unakuta kuna popo, lakini pia zimejaa mahabusu.  Ningeomba waziri alete mapendekezo tubadilishe sheria ili ambao wana makosa madogo wapigwe hata makofi tu na waachiwe,” alisema Msukuma.Akizungumzia mauaji na utekaji, Msukuma alisema:

“Sisi kama wabunge tunaotunga hizi sheria tuviache vyombo vifanye kazi yake, hawa wanaosema sijui nani kapotea mara Beny Saanane, hata watu wa CCM wamepotea wengi tu, wamechinjwa Kibiti wengi tu, na hatukupiga kelele, tumeviachia vyombo vinalishughulikia.“Mimi nilikuwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo pale Kinondoni, nani hajui kama mlikuwa mnasema kwamba watu waandamane na mbebe majeneza mia mbili?  Ungekuwa wewe serikali ungeacha watu waandamanae wafe? Tuviachie vyombo vifanye kazi yake, hata mimi nilifanya kosa na niliwekwa ndani. Hawa wakorofi wakifanya makosa wawekwe magerezani, unamuona Lema sasa hivi kidogo amekuwa binadamu.” 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search