Sunday, 8 April 2018

Mwandishi Finnigan wa Simbeye wa The Guardian aokotwa akiwa hajitambui, amepigwa vibaya jijini Dar

Wananchi wa Bunju wamemwokota ndugu Finnigan wa Simbeye wa The Guardian akiwa hajitambui.

675cf91f-663f-4e8c-b8a3-43830ad4a184.jpg 
5B464BFE-D7F6-488E-B017-0906FCA243B4.jpeg 
Mmoja wa wahariri waandamizi wa gazeti la The Guardian, Finnigan Simbeye ameokotwa eneo la Bunju wilayani Kinondoni akiwa hajitambui.


Taarifa zilizosambaa leo Jumapili Aprili 8, 2018 kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kitambulisho chake cha kazi cha kampuni ya The Guardian Limited zinaeleza Simbeye aliokotwa akiwa kwenye hali mbaya.


Hata hivyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne alipotafutwa na MCL Digital amesema hana taarifa za tukio la kuokotwa Simbeye.


Rose Mirondo, ambaye ni mkewe Simbeye amesema mumewe aliondoka nyumbani jana Jumamosi Aprili 7, 2018 akiwa na gari lakini hakurudi hadi alipopata taarifa za kuokotwa kwake leo.


Amesema alipokwenda eneo la tukio Bunju hakuliona gari wa mumewe.

Rose amesema watu aliowakuta eneo la tukio wamemweleza kwamba Simbeye alichukuliwa na polisi kupelekwa hospitali.

Amesema bado hana taarifa ya hospitali gani amepelekwa na kwamba, anakwenda Kituo cha Polisi Bunju kupata taarifa zaidi.
Na Bakari Kiango, Mwananchi

For the English AudienceFinnigan F. Simbeye, a seasoned Journalist and Revised Editor for The Guardian, a Tanzanian newspaper has been found unconscious and wounded at Bunju in Dar es Salaam.

Witnesses say his injuries suggest he faced a serious beating. He has been rushed to Mwananyamala hospital while the responsible party remains a mystery.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search