Tuesday, 24 April 2018

MWIGIZAJI NCHINI NIGERIA ATANGAZA KUGOMBE AURAIS

Muigizaji wa filamu wa Nigeria Yul Edochie ambaye pia ni mtoto wa muigizaji maarufu na mkongwe wa nchini humo Pete Edochie, ametangaza kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi ujao mwaka 2019.

Yul ametangaza uamuzi huo leo hii kupitia ukurasa wake wa twitter, akisema kwamba umefika wakati sasa wa kusitisha uongozi mbaya wa viongozi waliopo kwenye nchi hiyo.

“Leo natangaza malengo yangu ya kugombea Urais wa nchi hii bora zaidi duniani Nigeria, nchi iliyobarikiwa iliyoumizwa kwa miongo kadhaa na viongozi wabaya. Inatosha!! Wanaigeria wenzangu, simameni na mimi, tufikishe matatizo yetu kwenye kituo cha mwisho cha basi”, ameandika Yul Edochie.

Azimio lake limeonekana kuvutia sana vijana ambao walihukumu taarifa ya Rais Muhammadu Buhari katika Mkutano wa Biashara wa Jumuiya ya Madola, akisema vijana wengi wa nchi hiyo ni wavivu.

Yul alishawahi kugombea ugavana wa jimbo la Anambra mwaka 2017, lakini alishindwa na safari hii kutangaza nia kwenye nafasi hiyo kubwa ya uongozi wa nchi.

Nigeria inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa Urais mwaka 2019 huku Rais wa sasa wa nchi hiyo Muhammadu Buhari akitarajiwa kugombea, licha ya misukosuko mingi na lawana anazopewa na Wanaigeria kwa kuyumbisha uchumi wa nchi hiyo.Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search