Thursday, 5 April 2018

NAIBU SPIKA ATOA NENO KUHUSU KAMPUNI YA PHILIPS

Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson ameitahadharisha Serikali kuwa makini na kampuni ya Philips ambayo imeingia nayo mkataba wa kutoa huduma za XRays nchi nzima kwa madai kwamba ni wasumbufu.


Naibu Spika ametoa kauli hiyo jana wakati Naibu Waziri wa Afya Dk. Faustine Ndugulile alipoweka wazi kuwa Serikali inatarajia kuingiza nchini machine 34 za kisasa za XRay ambazo zitaletwa na kampuni hiyo ya Philips.


Dk. Tulia alisema kuwa kampuni hiyo ilisumbua sana katika tenda ya Hospitali ya Mafia, iliyosababisha Mafia kutokuwa na Mashine mwaka mzima hivyo kuiomba wizara kujipanga vizuri kwani wana usumbufu mkubwa.


Akitaka kupata uhakika juu ya kampuni hiyo Dkt. Tulia alisema; "Mh. Naibu Waziri naomba utufafanulie vizuri kampuni hii ndiyo ile iliyowasumbua hospitali ya Mafia kwa mwaka mzima ni hawa philips au siyo hawa? 


"Kama ni hawa utatufafanulia baadaye lakini kama ni hawa wameshatusumbua sana. Mbunge wa Mafia ameshazungumza sana humu ndani".


Akifafanua kuhusu kampuni hiyo Naibu Waziri wa Afya alisema kuwa serikali kupitia wizara imeingia mkataba wa utoaji wa huduma za Xrays nchi nzima na kampuni hiyo pasipo kukweka wazi kama ndiyo hiyo kampuni inayolalamikiwa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search