Friday, 20 April 2018

Naibu Waziri wa Fedha atoa kauli kuhusu kutoonekana kwa sh. Trilioni 1.5 kwenye ripoti ya CAG


Image result
Naibu waziri wa fedha, Ashatu kijazi ametoa kauli ya Serikali kuhusu kutoonekana kwa fedha kiasi cha Shilingi trilioni 1.5

Katika kipindi cha mwaka wa 2012/2013 hadi mwaka 2016/2017 serikali ilikuwa katikakipindi cha mpito cha kutekeleza mpango mkakati wa kuandaa mapato ya serikali kwa kutumia viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma, yaani International Public Sector Accounting Standards (IPSAS Accrual)

Katika kipindi hicho serikali ilitumia mfumo huo kukusanya hesabu za mapato na matumizi ya serikali kiwezesha kikamilifu kutambua hesabu za mali, madeni na makusanyo ya kodi

IPSAS Accrual ni mfumo ambao mapato na matumizi yanatambuliwa baada ya muhamala husika kukamilika na si hadi pesa taslimu inapopokelewa ama kutolewa

Matokeo ya utekelezaji wa mfumo huu umeiwezesha serikali kutoa taarifa za uwazi katika taasisi zake na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango

Amesema kuwa hakuna fedha ya kiasi cha trilioni 1.5 zilizopotea au kutumika bika kuidhinishwa na bunge, bali ni kutokana na serikali kutumia mfumo wa IPSAS Accrual

Taarifa ya CAG imeeleza jumla ya mapato yote ya serikali ni Shilingi Trilioni 25.3 kwa mwaka 2016/2017

Mapato haya ni pamoja na kodi , mapato yasiyo ya kodi, mikopo ya ndani na nje na misaada ya wahisani

Kuanzia mwaka wa 206/17 TRA ilianza kuutambua rasmi mfumo wa IPSAS Acrrual, katika mapato ya serikali ya mwaka huo wa fedha kulikuwa na mapato tarajiwa, yaani receivables ya jumla ya Shilingi bilioni 687.3 pamoja na mapato yaliyokusanywa kwa niaba ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya jula ya Shilingi bilioni 203.92

CAG alitumia taarifa za hesabu na nyaraka mbalimbali ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni ambapo mapato yalikuwa ni jumla ya Shilingi 25.3 na matumizi Shilingi trilioni 23.79

Matumizi haya hayakujumuisha Shilingi bilioni 697. 85 zilizotumika kulipa dhamana na hati fungani za serikali zilizoiva, matumizi haya yalikuwa hayajafanyiwa uhamisho wakati ukaguzi unakamilika

Hivyo baada ya kufanya uhamisho jumla ya matumizi yote kwa kutumia ridhaa za matumizi yalikuwa ni shilingi trilioni 24.4

Shilingi trilioni 1.54 zilizodaiwa kupotea zilitokana na mchanganuo ufuatao

Matumizi ya hati fungani zilizoiva Trilioni 0.6979

Mapato tarajiwa (Receivables) Trilioni 0.6873

Mapato ya Zanzibar Trilioni 0.2039

Jumla Trilioni 1.5891
Punguza Bank Overdraft Trilioni 0.0791

Fedha amabyo haijaonekana Trilioni 1.511.jpg
2.jpg
3.jpg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search