Saturday, 7 April 2018

RAIS MAGUFULI: MKE WANGU NI MTOTO WA POLISI, MAISHA YAO NAYAJUARais John Magufuli akiwa jijini Arusha amezindua nyumba za Jeshi la Polisi na ametaka watu ambao waliounguliwa nyumba zao kesho wahamie wasije kuhamia maofisa na wao kuachwa.

Pia amesema maisha ya Polisi anayajua kwani ndiyo yaliyomtunzia mke kwani alikuwa mtoto wa askari Polisi.

Kwa sasa Rais Magufuli yuko uwanja wa Sheikh Amri Abeid akishuhudia umahiri na mazoezi ya Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu na opereshani zao mbalimbali. Fuatana nami kujua kinachijiri Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kwa upande wao polisi wameahidi unyang'anyi kwa kutumia pikipiki unaenda kuwa historia kwani wamejipanga na maonyesho yanafata ni ya kutuliza ghasia.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search