Friday, 6 April 2018

Spika Job Ndugai akiri kuyafahamu madai ya kambi ya upinzani bungeni, amwandikia Mbowe barua kuona namna ya kuyatatua

PIX1-Mhe.Spika-akiongoza-Bunge-1-750x375.jpg 


Spika akiri kuyafahamu madai ya upinzani bungeni

Spika wa bunge Job Ndugai ameongea na #AZAMTV na amesema madai yaliyotolewa jana na Mbowe (KUB) anayafahamu na atayafanyia kazi na hivyo amechukua hatua ya kumwandikia Mbowe barua ili wakutane na waone wanalimalizaje suala hilo ili kuweza kufanya shughuli za bunge na hasa bunge la Bajeti linafanyika kama ilivyopangwa.

Kauli hii ya spika inakuja siku moja baada ya Mbowe kutoa malalamiko ya wafanyakazi wa ofisi ya KUB kuondolewa na ofisi ya spika na hivyo kukosa wataalamu na kushindwa kuandaa hotuba na kuchambua kwa ajili ya kuwasilisha katika bunge la bejeti linaloendelea. Kutokana na kuondolewa kwa wafanyakazi hao ambao walikuwa wanasaidia kufanya utafiti na kuandaa hotuba, kambi ya upinzani ilitangaza kuacha kuandaa hotuba mbadala katika bunge la bajeti linaloendelea.

Pia Mbowe aliotoa malalamiko ya kunyimwa stahili zake kama KUB toka mwezi January, kuondolewa dereva ambaye kisheria alipaswa kulipwa na bunge lakini haifanyiki hivyo.

Spika Ndugai amezungumzia suala la matibabu ya Lissu kuwa bado lipo kwenye mchakato,na wakati ukifika, basi bunge lilalitolea ufafanuzi.

Ndugai anasema Lissu alifanya "self referral" ya kutoka Dodoma kwenda Nairobi ambayo ni kinyume na utaratibu wa kawaida wa matibabu wa viongozi na hata raia wa kawaida,maana kwa utaratibu alipaswa kuandikiwa rufaa hiyo na daktari.

Spika anasema kinyume chake ni kuwa maamuzi ya rufaa ya Lissu kwenda Nairobi na hatimaye Ubelgiji ilikuwa ni maamuzi ya ndugu,familia na chama chake na sio madaktri,na ndio maana hata bunge lilishindwa kuidhinisha pesa sababu utaratibu haukufuatwa na hii ndio ilisababisha wabunge wamchangie pesa toka mifukoni mwao kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa mbunge mwingine yoyote.

Kuhusu suala la kuimarishwa kwa ulizni kwa Wabunge wawapo Dodoma, Spika Ndugai anasema kuwa Dodoma haiitaji ulinzi wa ziada kwa wabunge kwasababu Dodoma ni salama na tukio la kupigwa Lissu lilikuwa la "kipekee" na haliwezi kujirudia tena, hivyo wabunge na wananchi wasiwe na wasiwasi na usalama wao wawapo Dodoma.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search