Thursday, 19 April 2018

Spika Job Ndugai ataja sifa za mbunge kutibiwa nje ya nchi

lissu+pic.jpg
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ili mbunge aweze kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za Bunge anapaswa kuwa na vibali vitatu; kibali cha Bunge, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Rais John Magufuli.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliyehoji sababu za Bunge kushindwa kutoa gharama za matibabu za mbunge wa chama hicho Singida Mashariki, Tundu Lissu.

"Kuna siku nitataja orodha ya wabunge wanaotibiwa nje ya nchi. Ni lazima wawe na vibali hivi. Rais alishasema wazi kuwa anazuia safari za nje zisizokuwa na lazima. Lissu alipelekwa Nairobi katika matibabu kwa utaratibu ambao haukuwa na kibali cha Bunge. Hili jambo nimeshalisema sana sijui kwanini linajirudia, "amesema na kuongeza:

“Nashukuru Lissu anaendelea na matibabu na ninajua kuna Wajerumani wanamsaidia."Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search